AI NA AJIRA: JE, VIJANA WATAKOSA KAZI AU WATAPATA FURSA MPYA?
Kuna
swali ambalo linazidi kusikika kila mahali:“Kama AI inaweza kufanya kazi
ambazo mwanadamu alikuwa anafanya, tutapata wapi ajira?”Swali hili si la
kufikirika. Tayari kuna watu wanaona mabadiliko katika maeneo yao ya kazi. Kazi
ambazo zamani zilihitaji watu kadhaa sasa zinaweza kufanyika kwa kutumia
kompyuta, simu na zana za akili bandia.Lakini kuna upande mwingine ambao mara
nyingi hauzungumzwi.Wakati teknolojia inapunguza mahitaji ya baadhi ya kazi,
mara nyingi huleta pia aina mpya za kazi ambazo hazikuwepo hapo awali.Ndiyo
maana jambo kubwa si kujiuliza tu, “AI itachukua kazi yangu?” Swali
muhimu zaidi ni:“Ninawezaje kujifunza kuitumia AI kabla haijabadilisha
kabisa namna kazi yangu inavyofanyika?”
KAZI ZINABADILIKA, SI LAZIMA ZITOWE
ZOTE
Historia
imetufundisha kwamba teknolojia inapokuja, baadhi ya kazi hubadilika.Mashine za
viwandani zilipunguza baadhi ya kazi za mikono, lakini zikaongeza mahitaji ya
mafundi, wahandisi, waendeshaji wa mashine na wataalamu wengine.Kompyuta
zilipoingia maofisini, baadhi ya kazi za kuandika kwa mkono zilipungua.Lakini
zikazaliwa kazi zinazohusiana na programu, mitandao, usimamizi wa data na
huduma za kidigitali.AI nayo iko katika mchakato huo.Inaweza kufanya kazi
fulani kwa haraka sana, lakini bado kuna mambo ambayo yanahitaji mtu kuelewa
mazingira, watu, maadili, uwajibikaji na matokeo ya uamuzi.Kwa hiyo, si sahihi
kusema kwamba kila mtu atapoteza kazi kwa sababu ya AI.Lakini pia si busara
kusema kwamba hakuna kazi yoyote itakayoathirika.Mabadiliko yatatokea.Na
wale watakaokataa kujifunza wanaweza kujikuta wakishindanishwa na watu
wanaotumia teknolojia kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
MFANYAKAZI
WA KAWAIDA ANAWEZA KUTUMIA AIJE?
Hebu
tumchukue mtu anayefanya kazi ya ofisini.Anaweza kutumia muda mwingi kuandika
barua, kutengeneza ripoti, kupanga taarifa na kuandaa mawasiliano.AI inaweza
kumsaidia kuandaa rasimu ya barua, kupanga mawazo au kufanya muhtasari wa
taarifa.Lakini bado mtu huyo ndiye anayepaswa kuhakikisha taarifa ni sahihi na kwamba
ujumbe unafaa kutumwa.Hapo AI haijawa mfanyakazi wake.Imekuwa chombo cha
kuongeza uwezo wake.Hii ndiyo tofauti ambayo watu wengi bado
hawaioni.Tatizo si kwamba mtu anatumia AI.Tatizo linaweza kuwa mtu mwingine
anatumia AI vizuri zaidi kuliko yeye.
VIJANA WANA
FURSA KUBWA
Kwa
vijana, mabadiliko haya yanaweza kuwa changamoto lakini pia ni fursa.Kijana
ambaye hana mtaji mkubwa anaweza kuanza kujifunza ujuzi wa kidigitali kwa
kutumia simu.Anaweza kujifunza:
- Kuandika
maudhui
- Kutengeneza
tovuti
- Kutafsiri
- Kuhariri
video
- Kutengeneza
picha
- Kusimamia
mitandao ya kijamii
- Kutengeneza
matangazo
- Kufanya
utafiti
- Kuandaa
nyaraka
- Kufundisha
watu kutumia zana za AI
Hapa
ndipo tunapaswa kubadilisha namna tunavyofikiria kuhusu ajira.Si lazima kila
kijana asubiri kampuni imwajiri.Baadhi wanaweza kujenga huduma zao na
kuwahudumia wengine.
MFANO WA MTU
MWENYE SIMU TU
Tuchukulie
kijana mwenye smartphone na internet.Anaweza kujifunza kutengeneza posters kwa
kutumia programu za ubunifu.Baada ya kujifunza, anaweza kuanza kutengeneza
matangazo kwa wafanyabiashara wadogo.Duka linahitaji poster ya ofa.Mgahawa
unahitaji tangazo.Kanisa linahitaji poster ya mkutano.Mwalimu anahitaji tangazo
la kozi.Kijana huyo anaweza kuanza kupata wateja mmoja baada ya mwingine.Hakuwa
na ofisi kubwa.Hakuwa na printer.Hakuwa na kampuni kubwa.Alianza na ujuzi na
simu.AI inaweza kumsaidia kuongeza kasi ya kazi yake, lakini thamani kubwa
bado iko katika uwezo wake wa kuelewa kile mteja anahitaji.
KILE AI
HAIWEZI KUKUPATIA
Kuna
jambo muhimu sana ambalo vijana wanapaswa kulielewa.AI inaweza kukupa
taarifa, lakini haiwezi kukupa uzoefu wa maisha kwa siku moja.Haiwezi
kukufanya uwe mwaminifu kwa kukupa paragraph kuhusu uaminifu.Haiwezi kukufanya
uwe mfanyabiashara mzuri kwa kukupa mpango wa biashara pekee.Haiwezi kukufanya
uwe kiongozi mzuri kwa kukuandikia hotuba.Haiwezi kuchukua nafasi ya miaka ya
kujifunza watu, kufanya makosa, kurekebisha makosa na kujenga uaminifu.Kwa
hiyo, mtu anayejua AI lakini hana nidhamu, hana uaminifu na hajui kushirikiana
na watu bado anaweza kushindwa.Ujuzi wa teknolojia unahitaji kuambatana na
tabia nzuri.
AJIRA
ZITAZIDI KUTAKA MTU ANAYEJUA VITU VINGI
Zamani
mtu angeweza kuajiriwa kwa sababu alikuwa na ujuzi mmoja maalumu.Katika
mazingira mapya, mwajiri anaweza kutafuta mtu anayejua zaidi ya kitu kimoja.Kwa
mfano:Mtu anayejua kuandika + kutumia AI + kutengeneza maudhui anaweza kuwa na
uwezo mpana kuliko mtu anayejua kuandika pekee.Mtu anayejua biashara + digital
marketing + AI anaweza kujenga huduma yenye nguvu zaidi.Mwalimu anayejua
kufundisha + kutumia teknolojia anaweza kuwafikia wanafunzi wengi
zaidi.Mchungaji anayejua Biblia + mawasiliano + teknolojia anaweza kufikisha
ujumbe kwa watu ambao hawafiki kanisani.Hii haimaanishi kila mtu lazima awe
mtaalamu wa teknolojia.Inamaanisha kwamba ujuzi tofauti unapounganishwa,
thamani ya mtu inaweza kuongezeka.
KWA NINI
BAADHI YA WATU WATAATHIRIKA ZAIDI?
Kazi
zinazotegemea sana kurudia jambo lilelile zinaweza kuwa katika hatari kubwa
zaidi ya kuendeshwa na automation.Mfano unaweza kuwa kazi zinazohusisha:
- Kuingiza
taarifa zinazojirudia
- Kuandaa
maandishi ya kawaida
- Kujibu
maswali yale yale
- Kuchambua
taarifa rahisi
- Kazi fulani
za utawala
Lakini
hata hapa, mabadiliko hayatokei kwa siku moja.Kampuni nyingi bado zinahitaji
watu kusimamia mifumo, kukagua makosa na kufanya maamuzi.Kwa hiyo, mtu
anayefanya kazi ya aina hii hapaswi kuogopa tu.Anapaswa kuanza kuuliza:“Ni
sehemu gani ya kazi yangu inaweza kujiendesha, na ni sehemu gani ninahitaji
kuwa bora zaidi?”
Hilo ni
swali lenye nguvu kuliko kuishi kwa hofu.
No comments:
Post a Comment