KANISA LA BAADAYE LITAHITAJI WATUMISHI
WANAOJUA TEKNOLOJIA
Hatuwezi
kujifanya dunia haitabadilika.Watoto wanaokua leo watatumia teknolojia
zaidi.Vijana watatumia AI katika kazi zao.Biashara zitatumia automation.Elimu
itabadilika.Mawasiliano yatabadilika.Kwa hiyo Kanisa linahitaji viongozi
wanaoweza kuelewa dunia hiyo bila kupoteza misingi ya imani.Tunahitaji kizazi
cha watumishi ambao wanaweza kusema:“Ninaelewa teknolojia, lakini teknolojia
siyo Mungu wangu.”Huo ni uwiano tunaouhitaji.
MUNGU
ANAWEZA KUTUMIA TEKNOLOJIA, LAKINI TEKNOLOJIA SI MUNGU
Hili ni
jambo la mwisho ambalo ningependa tulifikirie.Katika historia, Mungu amekuwa
akitumia njia mbalimbali kuwafikia watu.Lakini njia siyo Mungu.Kitabu si
Mungu.Redio si Mungu.Television si Mungu.Internet si Mungu.AI si Mungu.Hivi ni
vyombo.Kwa hiyo tusiviabudu.Tusiviogope kupita kiasi.Tutumie kwa hekima.
HITIMISHO:
TUITUMIE AI, LAKINI TUSIPOTEZE ROHO YA HUDUMA
Kanisa
halipaswi kukimbia teknolojia.Lakini pia halipaswi kuacha teknolojia itawale
huduma.AI inaweza kusaidia sana katika uandishi, elimu, tafsiri, mawasiliano,
utafiti na utengenezaji wa maudhui.Lakini mambo muhimu zaidi ya huduma hayawezi
kubebwa na AI:
Maombi.
Upendo.
Imani.
Uaminifu.
Ushirika.
Huruma.
Maisha yaliyobadilishwa.Kwa hiyo tunapoingia katika kizazi
cha AI, Kanisa linapaswa kuwa na mikono miwili.Mkono mmoja ushike teknolojia
na maarifa.Mkono mwingine ushike Neno la Mungu na misingi ya imani.Tusikubali
teknolojia iturudishe nyuma.Lakini pia tusikubali teknolojia ituchukue mahali
ambapo Mungu hakutuita.Tuitumie AI kama chombo.
Tuitumie kwa hekima.
Tuitumie kwa ukweli.
Tuitumie kuwasaidia watu.
Na juu
ya yote:Tusiache teknolojia itusaidie kufanya kazi ya Mungu huku tukisahau
kuwa na uhusiano na Mungu mwenyewe.Kwa sababu Kanisa halihitaji tu
teknolojia yenye nguvu.Kanisa linahitaji watu wenye nguvu katika imani,
wenye hekima, wenye upendo na wenye moyo wa kumtumikia Kristo.
No comments:
Post a Comment