Badala
ya kuwakataza vijana kutumia teknolojia, Kanisa linaweza kuwa sehemu ya
kuwaelimisha.
Semina
za kanisa zinaweza kuwa na mada kama:
“AI na Maisha ya Mkristo.”
“Jinsi ya kutumia AI kwa masomo.”
“AI na ujasiriamali.”
“AI na maudhui ya Kikristo.”
“AI, maadili na ukweli.”
Hii
inaweza kusaidia vijana kuona kwamba imani na teknolojia si lazima viwe maadui.
AI INAWEZA
KUSAIDIA KANISA KUWAFIKIA WATU WENGI
Kanisa
dogo linaweza kuwa na ujumbe mkubwa.Mhubiri anaweza kuwa na simu tu na kuanza
kutengeneza maudhui.AI inaweza kusaidia kupanga maudhui hayo.Video moja inaweza
kufika kwa mtu ambaye hajawahi kuingia kwenye jengo la kanisa.Makala moja
inaweza kusomwa na mtu aliye nchi nyingine.Podcast inaweza kusikilizwa na mtu
akiwa safarini.Hii ni fursa kubwa.Lakini tusisahau:Reach siyo sawa na
transformation.Kuwa na views nyingi si lazima kumaanishe watu wengi
wamebadilika.
AI ISITUMIKE
KUPIMA THAMANI YA HUDUMA
Mtego
mwingine ni kuanza kuamini:
“Video
yangu imepata views 100,000, kwa hiyo Mungu yuko pamoja nami.”
Au:
“Mahubiri
yangu yamepata likes nyingi, kwa hiyo yalikuwa na nguvu.”
Si
lazima.Mitandao hupima engagement.Mungu anaangalia moyo na uaminifu.Huduma
inaweza kuwa na watu wachache lakini ikawa na matokeo makubwa katika maisha
yao.Kwa hiyo usiache metrics za internet ziwe kipimo cha mwisho cha huduma.
No comments:
Post a Comment