Mbinu za Kujilinda Dhidi ya WhatsApp Scams
Tumia kanuni hii rahisi:
STOP
S — Simama.
Usichukue hatua haraka.
T — Tafakari.
Jiulize kama ujumbe una mantiki.
O — Ondoa shaka.
Thibitisha taarifa kupitia chanzo kingine.
P — Protect.
Usitoe code,PIN,password au pesa bila uhakika.
WhatsApp kwa Biashara: Tahadhari Zaidi
Kama unatumia WhatsApp
Business, usalama ni muhimu zaidi.Akaunti ya biashara inaweza kuwa na:
- wateja;
- contacts;
- order information;
- mawasiliano;
- taarifa za bidhaa;
- taarifa za malipo.
Mtu akipoteza udhibiti wa
akaunti ya biashara, madhara yanaweza kuwa makubwa.Kwa hiyo wafanyabiashara
wanapaswa kuwafundisha wafanyakazi wao kutambua phishing na scams. Wazazi Wanapaswa Kuwafundisha Watoto Nini
Kuhusu WhatsApp?
Watoto wanapaswa
kufundishwa:
- kutowapa watu strangers taarifa binafsi;
- kutobofya links zisizojulikana;
- kutotuma picha binafsi kwa watu wasiowaamini;
- kutokutana na mtu waliyejuana naye online bila usalama
na ushirikishwaji wa mzazi/mlezi;
- kuripoti ujumbe wa kutisha au wa ajabu;
- na kutunza passwords na codes.
Elimu ya usalama wa
mtandao inapaswa kuanza mapema.
WhatsApp na Privacy: Kwa Nini Ni Muhimu?
Privacy haimaanishi kuwa
una kitu cha kuficha.Privacy ni uwezo wa kuamua:Nani anajua nini kuhusu
wewe? Katika dunia ya kidigitali, taarifa zako zinaweza kuwa na thamani.Jina
lako, namba yako,picha zako,contacts na taarifa zako nyingine zinapaswa
kushughulikiwa kwa uangalifu.
No comments:
Post a Comment