content='cf7ea80d2b8f4a87c4eb7cab715823fb' name='monetag'/> Smart pesa online: Jinsi ya Kulinda WhatsApp Yako

Monday, September 7, 2026

Jinsi ya Kulinda WhatsApp Yako

 

Jinsi ya Kulinda WhatsApp Yako

Sasa tumeona mambo ambayo hupaswi kufanya.Hebu tuangalie hatua za msingi unazoweza kuchukua.

1. Washa Two-Step Verification

Fungua WhatsApp na uangalie sehemu ya:

Settings → Account → Two-step verification

Kisha fuata maelekezo ya kuweka PIN.Kumbuka PIN yako na usimpe mtu mwingine.

2. Kagua Linked Devices

Nenda kwenye:

Settings → Linked Devices

Angalia vifaa vilivyounganishwa.Kama kuna kifaa usichokijua, chunguza na ukiondoe ikiwa ni lazima.

3. Kagua Privacy Settings

Nenda kwenye:

Settings → Privacy

Kisha pitia chaguo mbalimbali.Usiache mipangilio yako bila kuijua.

4. Linda Simu Yako

WhatsApp ikiwa salama lakini simu yako iko wazi, bado unaweza kuwa katika hatari.Tumia screen lock.Usimpe mtu PIN yako.Usishiriki biometric access yako.

WhatsApp Scam Ni Nini?

WhatsApp scam ni udanganyifu unaotumia WhatsApp kama njia ya kumshawishi mtu kutoa pesa,taarifa binafsi,credentials au kufanya kitendo kinachomnufaisha scammer.

Scams zinaweza kuja kwa njia tofauti.Mfano:

·       Scam ya pesa

“Rafiki yangu,nimepata tatizo.Nitumie pesa.”

·       Scam ya zawadi

“Hongera! Umeshinda zawadi.”

·       Scam ya kazi

“Tumekuchagua kupata kazi ya online.”

·       Scam ya investment

“Wekeza leo na upate faida kubwa ndani ya masaa machache.”

·       Scam ya verification

“Nitumie code niliyotumiwa kimakosa.”

Usikubali ujumbe kama huo bila kuthibitisha.

WhatsApp Phishing Ni Nini?

WhatsApp phishing ni mbinu ya kumdanganya mtumiaji ili afungue link au atoe taarifa.Scammer anaweza kutengeneza ujumbe unaofanana na mawasiliano ya kampuni halali.Lengo linaweza kuwa:

  • kuiba login details;
  • kuiba taarifa binafsi;
  • kukupeleka kwenye tovuti fake;
  • kukushawishi utume pesa;
  • au kukufanya upakue programu hatari.

Kwa hiyo, usiamini link kwa sababu tu imetumwa kwenye WhatsApp.

No comments:

Post a Comment